Kumekucha Huko...Divathebawse Atangaza Kwenda Uturuki Kufanya Operation ya Shingo Awe Kama Beyonce


Ni Headlines za mtangazaji maarufu wa kipindi cha LaviDavi ya Wasafi FM @divatheebawse , ambae amefunguka exclusive ,kuhusu kwenda nchini uturuki kwa ajili ya kufanya surgery/upasuaji wa kupunguza nyama ya shingo na kurefusha shingo yake ,ili kupata muonekano kama wa mwanamuziki wa marekani @beyonce.

Kwenye exclusive interview aliyofanya nasi, #Diva ameeleza kuwa licha kushawishika na muonekano wa beyonce, pia mdogo wake Sharon Malinzi ndie mtu pekee ambae amekua akimsisitiza kupata muonekano kama wa queen Bee' ili asizeeke na kubaki na katika muonekano wake wa umri mdogo.

Mbali na hayo mtangazaji huyo ameeleza kuwa tayari amesha-anza kufanya diet na kufanya vitu vya kumfurahisha mdogo wake, huku akieleza kuwa gharama za kufanya upasuaji uturuki sio kubwa hivyo siku si nyingi anakwenda kuwa kama beyonce.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad