Kwanini Timu Nyingi Zinapata Tabu Mwanzoni Mwa Ligi? Simba Mfano




Nilipofika Jijini Dodoma kwenye mchezo wa Dodoma Jiji na Simba nilipata wasaa wa kukaa na Watalaam mbalimbali, kuna Kocha mmoja mkubwa nilimuuliza swali

Kocha kwanini Simba huwa wanaanza msimu wakiwa hawapo imara, misimu zaidi ya mitatu sasa! Mwalimu yule wa timu tofauti na Simba akaanza kunipa elimu yake

Kwanza hoja ya KUTUMIKA! akaniambia 80% ya wachezaji wa Simba ni wa timu za taifa, 80% ya wachezaji wa Simba wamecheza mechi zaidi ya 40 hapo uchovu ni lazima ndio maana waaanza taratibu

Hii ni hoja ya uchovu, akaniambia ina maana kubwa sana! Hivyo Mwalimu analazimika kufanya rotation mpaka maeneo hatarishi ili kubalance vyema mzigo huo! Wachezaji wao wametumika sana

Hapo nikamuelewa Mwalimu yule kwenye hoja hiyo, yeye anasema suala sio chemistry, anasema ni suala la muda tu watapick kuanzia game ya tano

Nikataka kujua kwanini wachezaji wa Simba wanaumia sana? Safari yangu Dodoma ilinipeleka kwa Daktari mmoja wa timu ya Ligu kuu maeneo ya shule ya Sekondari, John Mallen baada ya stori kadhaa nikamuuliza hilo swali

Akaanza kwa kucheka kidogo na kuniambia hapa nakujibu kama Mwanataaluma sio Daktari wa timu flani, kisha akaanza kutoa nondo "ukiona Wachezaji wanaumia sana na wanaanza kwenye gia ndogo maana yake hao wamefanya Pre season ya kweli kabisa"

Akaniambia kuna kitu kinaitwa WATER THERAPY kitaalamu kabisa! Akaniambia Wachezaji wanapoingizwa sana kwenye barafu ni kuwa wanafanyiwa Natural healing, yani kujua sehemu mbalimbali za majeraha yao mwilini

Akaniambia Simba wanafanya sana WATER THERAPY, ikumbukwe hata kama una maumivu ya miaka 10 iliyopita kupitia hii itagundulika na utapewa tiba sahihi, sasa ile tiba huwa ina muda kabla wachezaji kukaa sawa

Nikahoji hapo hapo!.....


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad