Leo ni Leo..Hukumu Kesi ya Sabaya na Wenzake leo




Je, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya atashinda kesi ya unyang’anyi wa kutumia silaha inayomkabili au ataanza safari ya maisha jela kwa muda usiopungua miaka 30?
Majibu ya swali hili yanatarajiwa kutolewa leo na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha, Odira Amworo baada ya kusikiliza kesi dhidi ya Sabaya na wenzake wawili kwa miezi miwili na nusu iliyopita.

Hatima ya Sabaya inasubiriwa kwa hamu na watu wengi kutokana na umaarufu aliojipatia wakati akiwa Mkuu wa Wilaya ya Hai na jinsi staili yake ya uongozi iliyowagusa watu wengi kwa namna tofauti.

Tangu kufikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Julai 2, kesi dhidi ya Sabaya imekuwa ikivuta watu wengi wa jiji la Arusha na maeneo ya jirani ambao wamekuwa wakijitokeza mahakamani kuisikiliza.


OPEN IN BROWSER
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad