MAELFU Ya watu duniani wanatumia mtandao maarufu wa WhatsApp kuwasiliana na ndugu, jamaa na watu wao wa karibu kwa meseji na video lakini watu wengi watashindwa kuitumia huduma hiyo kutokana na mifumo ya simu zao kuanzia mwezi Novemba mwaka huu.
Kwa mujibu wa ripoti zilizotolewa na chapisho la 'The Sun' la nchini Uingereza limeeleza kuwa program ya WhatsApp haitafanya kazi wa baadhi ya simu janja kuanzia Novemba 2021.
Kwa mujibu wa chapisho hilo imeelezwa kuwa program hiyo haitafanya kazi kwa baadhi ya simu za iPhone na Android na watumiaji wa simu hizo wameshauriwa kununua simu mpya au kusasisha simu zao (software updating.)
Imeelezwa kuwa aina 40 za simu janja hazitapata huduma hiyo huku huduma ya kusasisha ( software updating,) kwa watumiaji wa simu hizo utafikia ukomo Novemba mosi mwaka huu.
Ili watumiaji kuweza kutumia huduma hiyo watumiaji wa simu za Android wanatakiwa kutumia Android 4.1 na zaidi na watumiaji wa iPhone kutumia iOs 10 na zaidi.
Simu ambazo zitakosa huduma ya WhatsApp kuanzia Novemba ni pamoja na :
iPhone
iPhone 5
iPhone 6S Plus
iPhone SE
Samsung
Galaxy Trend Lite
Galaxy Trend II
Galaxy SIII
Galaxy S3 Mini
Galaxy Xcover 2
Galaxy Core
Galaxy Ace 2
LG
Lucid 2
Optimus F7
Optimus F5
Optimus L2 II Dual
Optimus L5
Best L5 II
Optimus L5 Dual
Best L3 II
Optimus L7
Optimus L7 II Dual
Best L7 II
Optimus F6, Enact
Optimus L4 II Dual
Optimus F3
Best L4 II
Best L2 II
Optimus Nitro HD
Optimus 4X HD
Optimus F3Q
ZTE
ZTE V956
Grand X Quad V987
Grand Memo
Sony
Xperia Miro
Xperia Neo L
Xperia Arc S
Huawei
Ascend G740
Ascend Mate
Ascend D Quad XL
Ascend D1 Quad XL
Ascend P1 S
Ascend D2
Other smartphones
Alcatel
Archos 53 Platinum
HTC Desire 500
Caterpillar Cat B15
Wiko Cink Five
Wiko Darknight
Lenovo A820
UMi X2
Run Fl1
THL W8