WANASAYANSI kutoka Marekani wamefanikiwa majaribio ya kupandikiza Figo ya Nguruwe kwa Binadamu na kugundua kuwa kiungo hicho kinaweza fanya kazi kikamilifu.
Wataalamu hao kutoka N.Y.U. Langone Health Taasisi ya kupandikiza Figo huko Manhattan wanasema walitoa Figo inayofanya kazi kwa Nguruwe kisha ikabadilishiwa vinasaba na kuipandikiza kwa Mwanadamu.
Hatua hiyo ya mafanikio inaweza kuleta matumaini kwa wagonjwa na kuwa chanzo endelevu na mbadala kwenye upatikanaji wa viungo hivyo.