Majina manne ya makocha hawa yatua mezani kwa Man United




Manchester United ina orodha ya majina manne ya kumrithi kocha wake aliyekalia kuti kavu Ole Gunnar Solskjær, hayo ni kwa mujibu wa chombo cha habari cha Sun.



Miongoni mwa majina hayo ya makocha yanayodaiwa ni pamoja na Zinedine Zidane, Antonio Conte, Meneja wa Leicester Brendan Rodgers na wa Ajax boss Erik ten Hag.

Lakini Meneja wa Paris St-Germain Muargentina Mauricio Pochettino, 49, anasalia kuwa chaguo namba moja la Manchester United kumrithi Solskjaer. (Star)

Newcastle wako tayari kumpa Ten Hag mshahara wa £6m kwa mwaka baada ya kodi na kufanya marupurupu yote kufikia £11m kwa mwaka lakini Mholanzi huyo, 51, amegoma kuondoka Ajax. (Mail)

Newcastle pia haijakata tamaa kumrejesha kocha wake wa zamani Rafael Benitez. Mhispania huyo, 61, kwa sasa anainoa Everton. (Football Insider)

b

Meneja wa zamani wa Roma Paulo Fonseca, 48, anatarajia kukubali ofa ya kuwa Meneja mpya wa Newcastle, lakini wamiliki wapya wa klabu hiyo bado wanatafakari uamuzi wao. (Fabrizio Romano, via Chronicle)

Barcelona bado wanamatumini ya kumpata kocha wa Liverpool Mjerumani Jurgen Klopp, 54, ili amrithi kocha wa sasa Ronald Koeman. (Sport – in Spanish)

Arsenal inahaha kumshawishi William Saliba kwamba maisha yake ya soka ni pale Emirates na wanaweza kulazimika kumuuza mlinzi huyo mfaransa, 20, ambaye ameonyesha kiwango cha kuvutia Marseille anapocheza kwa mkopo. (Sun)

Arsenal wanajiandaa kupambana na Manchester City katika mbio za kumsajili kama mchezaji huru mlinzi wa Hispania Sergi Roberto, 29 kutoka Barcelona . (Fichajes, via talkSPORT)

Kiungo wa Manchester United Donny van de Beek amemkataa wakala wa soka Mino Raiola baada ya wakala huyo kumuomba mholanzi huyo mwenye miaka 24 awe wakala wake mpya. (Mike Verweij, via Express)

Chelsea imepewa ofa ya kumsajili mlinzi wa Uholanzi mwenye miaka 22 Matthijs de Ligt wakati huu Juventus ikitaka kupunguza kiwango cha mishahara inayotoa kwa wachezaji. (Goal, via Star)

Aston Villa, AC Milan na Bayer Leverkusen ni miongoni mwa vilabu vinavyomtaka mshambuliaji wa River Plate Muargentina Julian Alvarez, 21. (CalcioMercato – in Italian)

Barcelona imemfahamisha winga wake Mfaransa Ousmane Dembele, 24, kwamba ana mwezi mmoja tu wa kukubali ofa yao mpya ya kuongeza mkataba wake wa sasa ambao unakoma mwishoni mwa msimu ujao.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad