Muhtasari
Ole Gunnar Solskjaer amedokeza kuwa Manchester United imetoka kwenye"wiki ngumu" baada ya kupata ushindi kutoka Tottenham Nuno EspÃrito Santo
Ole Gunnar Solskjaer amedokeza kuwa Manchester United imetoka kwenye"wiki ngumu" baada ya kupata ushindi kutoka Tottenham Nuno EspÃrito Santo
Ole Gunnar Solskjaer amedokeza kuwa Manchester United imetoka kwenye"wiki ngumu" baada ya kupata ushindi kutoka Tottenham Nuno EspÃrito Santo.
Cristiano Ronaldo alikuwa nyota wa mchezo huo, ambao ulitoa jibu kamili kwa kuchapwa mabao 5-0 na Liverpool wiki iliyopita kwenye Uwanja wa Old Trafford jambo ambalo lilizua maswali mengi kuhusu mustakabali wa Solskjaer.
Solskjaer bado hajatoka kwenye wakati mgumu , lakini Ronaldo aliyafanya maisha yawe ya raha zaidi kwa bosi wake kwa kuweka mpira wavuni kutoka kwa Bruno Fernandes dakika sita kabla ya mapumziko, ikifuatiwa na pasi ambayo alimtengenezea Edinson Cavani. sekunde moja baada ya dakika 64.
"Jambo muhimu zaidi kwa mashabiki, mimi na wachezaji ni kuwa kitu kimoja," alisema bosi huyo anaye tokea nchini Norway, ambaye timu yake ilipata ushindi wa kwanza katika mechi tano za Ligi Kuu.
"Imekuwa wiki ngumu kwangu na kwa wachezaji, klabu, mashabiki. Nimekaa mbali na kelele nyingi. Lakini unajua kinachoendelea huko nje na unajua lazima uwe kwenye kiwango cha juu.
"Kila wakati unapopoteza mchezo ni hisia mbaya zaidi duniani kama kocha au meneja. Tulihitaji wiki nzima kufanyia kazi utendaji huu."
Marcus Rashford alihitimisha mambo kwa kumaliza dakika nne kabla ya mechi kumalizika huku mashabiki wa Spurs wakilipuka kwa hasira dhidi ya Nuno na mwenyekiti wao Daniel Levy, huku kelele za "tunataka Levy atoke" zikivuma kwenye uwanja huo mkubwa.
Tottenham hawakuwa na kiwango kizuri cha Harry Kane kwenye mchezo na sintofahamu miongoni mwa mashabiki wao, ambao walimgeukia meneja Nuno alipomtoa Lucas Moura na kumuingiza Steven Bergwijn katika kipindi cha pili.
Ronaldo alionyesha kipaji na uwezo wake wa hali ya juu wakati tu Solskjaer na United walivihitaji zaidi katika mchezo ambao hawakupaswa kupoteza.
Akisaidiwa na Cavani, mshambulizi huyo wa Ureno aliongezea kiwango cha hali ya juu katika mchezo wa United ambao ulikuwa uboreshaji mkubwa kutokan na matokeo yasiyo ridhisha dhidi ya Liverpool, ingawa hilo halikuwa gumu na Spurs walishindwa kuonyesha upinzani.
Ronaldo alikuwa tishio mara kwa mara na harakati zake, kwa mashambuliyo ya mara kwa mara United wakitawala.