Mapadri 3000 wagundulika kuwadhalilisha watoto kingono tangu 1950, Ufansa




Takriban watu 3000 wanaowadhalilisha watoto kingono wamekuwa wakiendesha maovu yao ndani ya kanisa katoliki nchini Ufaransa tangu mwaka 1950, hii ikiwa ni kwa mujibu wa mkuu wa tume huru inayochunguza kashfa hiyo, aliyezungumza na shirika la habari la AFP siku kadhaa kabla ya ripoti ya uchunguzi kutolewa rasmi. 

Jean-Marc Sauve amesema uchunguzi wao umewagundua wadhalilishaji watoto kingono kati ya 2900 na 3200 wanaodaiwa kuwa mapadri na waumini wengine wa kanisa hilo. 

Sauve amesema ripoti yao iliyo na kurasa 2,500 itatolewa siku ya Jumanne baada ya miaka miwili na nusu ya uchunguzi uliojikita makanisani, mahakamani, ukusanyaji wa nyaraka za polisi pamoja na mahojiano waliofanyiwa walioshuhudia kashfa hizo. 

STORI ZAIDI za AINA HII Download Udaku Spesho App HAPA


Tume hiyo ilianzishwa mwaka 2018 na Baraza la maaskofu la Ufaransa CEF na Mkutano Mkuu wa maaskofu wa Ufaransa CORREF kutokana na idadi ya kashfa za udhalilishaji wa kingono zilizoitikisa kanisa katoliki nchini Ufaransa na ulimwengu kwa ujumla.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad