Mapya yaibuka ! Pichani Khoirul Anam mwanaume wa nchini Indonesia amefunga ndoa na rice cooker hilo ili liwe mkewe wake. Ndoa imefungwa tarehe 20 September 2021 ambapo bwanaharusi huyo alivaa mavazi rasmi na kupewa cheti cha ndoa kwa kuoa chombo hicho cha umeme kinachotumika kupikia wali. rice cooker hilo lilivalishwa mtandio katika siku hiyo muhimu kwa kwenda kuanza mapya ya ndoa
Khoirul Anam amesema yeye ni mweupe(fair), hapendi kuzungumza sana na pia anapenda kupika na amelipenda sana rice cooker hilo na kuamua kulioa kabisa liwe mke wake huku akilimwagia mabusu ya upendo
Baada ya ndoa hiyo iliyoowaacha watu midomo, jamaa huyo alijitosa mitandaoni kupost picha za siku yake hiyo muhimu kwa kufunga ndoa ingawa bado hajapost picha zao za fungate(honeymoon) na mkewe huyo