Marekani yazungumza na Waziri Mkuu aliyepinduliwa Sudan





Marekani imesema Waziri wake wa mambo ya nje, Antony Blinken, amezungumza kwa njia ya simu na Waziri Mkuu wa Sudan aliyeondolewa madarakani, kufuatia Kiongozi huyo Abdalla Hamdok kureja nyumbani.
Hamdok alikamatwa na kushikiliwa baada ya Jeshi kuendesha mapinduzi ya kiutawala siku ya Jumamosi.

Taarifa iliyotolewa inasema Blinken alikaribisha kuachiliwa kwa Hamdok na akarudia wito wake kwa wanajeshi wa Sudan kuwaachilia huru viongozi wote wa kiraia wanaoshikiliwa.

Maandamano ya kupinga mapinduzi hayo ya kijeshi yanaendelea , huku umati wa watu wakikusanyika katika mji mkuu wa Khartoum kuandamana na kufunga barabara.

Mapema, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan alitaka kuhalalisha mapinduzi hayo kwa kuwashutumu makundi ya wanasiasa kwa kuchochea raia dhidi ya vikosi vya jeshi.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad