Maafisa wa Afya wa Afrika na wale wa Umoja wa Mataifa wameonya juu ya uhaba mkubwa unaonyemelea wa sirinji bilioni 2 za sindano hususan katika mataifa ya kipato cha chini na kati duniani kote.
Shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto UNICEF limesema uhaba huo utaathiri kiasi cha sindano bilioni 2.2 ambazo hutumiwa mara moja.
Hali hiyo imechangiwa na ongezeko la usambazaji wa dozi za Covid-19 barani afrika, baada ya miezi kadhaa ya kusuasua kwa kampeni hiyo.
Naye mkuu wa shirika la afya duniani WHO kanda ya Afrika Matshidiso Moeti, amewaeleza waandishi wa habari leo kwamba uhaba huo wa sindano unaweza kudumaza maendeleo.
Baadhi ya mataifa barani afrika yakiwemo Afrika Kusini, Kenya na Rwanda yameshuhudia ucheleweshaji wa vifaa hivyo.