Mavazi ya ‘Squid Game’ Yatafutwa Zaidi Mitandaoni





Filamu ya Kikorea ya ‘Squid Game’ iliyoachiwa rasmi Septemba 17, 2021, hadi sasa inaongoza kwa  mavazi na vitu vilivyotumika katika filamu hiyo, kutafutwa kwa wingi mitandaoni (Internet) ili mavazi na vitu hivyo vitumike katika sikukuu ya Halloween.

 

Filamu ya Squid Game inayohusiana na michezo ya watoto sambamba na vifo vya wachezaji wa michezo hiyo wakisaka donge nono la fedha, imetikisa mno soko la filamu duniani ambapo kwa mujibu wa mtandao wa kuonesha filamu duniani Netflix, filamu hiyo hadi sasa imetazamwa na watu zaidi ya milioni 111 katika mtandao huo kote duniani.

 

Kama ulikuwa haufahamu kuhusu Sikukuu ya Halloween, ni kwamba; Hii ni sherehe inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 31 Oktoba ili kuwakumbuka watu, watakatifu na waliouwawa kwa sababu ya imani yao. Sherehe hizo huenda sambamba na watu kuvalia nguo za kuogofya (Kutisha) , kutaniana, kutembelea mahala kuliko na makaburi pamoja na kutembelea sehemu zisizokaliwa na watu. Pia watu husimuliana hadithi za kuogofya zinazowafanya wengine kushtuka.

 

Kwa upande wa Wakristo, husherekea Halloween kwa kuwasha mishumaa na kwenda kanisani wakiomba na kufunga ili kuwabariki wafu wao, filamu kama Spider, Joker na Harley Quinn zinashikilia nafasi za juu zikiongoza kwa idadi ya watu wengi waliotafuta mavazi na vitu vilivyotumika katika filamu hizo, kupitia Internet.

Cc;@bakarimahundu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad