Mbaroni kwa Tuhuma za Kutengeneza Vitambulisho Feki vya NIDA




 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Pwani linamshikilia Abdul Selemani mwenye umri wa miaka 27, Mluguru mfanyabiashara wa stationary mkazi wa Visiga wilaya ya Kibaha mkoa wa Pwani kwa kosa la kutengeneza nyara za serikali.

 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Wankyo Nyigesa amesema mnamo tarehe Oktoba 12, 2021 majira ya saa 11:38 jioni maeneo ya Visiga Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vilimkamata mtuhumiwa Abdul Seleman kwa kosa la kutengeneza na kuuza vitambulisho vya taifa NIDA kwa Tsh 10,000 kwa kila kitambulisho kimoja.

 

Aidha, mtuhumiwa huyo amekamatwa na vifaa mbali mbali ikiwemo vitambulisho vya taifa NIDA, computer mpakato, Pvc card, Desktop computer pamoja na flash disk alizokuwa akizitumia katika kazi hiyo

 

Mtuhumiwa huyo atafikishwa mahakamani mara baada ya upelelezi kukamilika.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad