Mbowe amtaja Mwalimu Nyerere mahakamani




Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa Chadema akiingia mahakamani
KIONGOZI wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema, Freeman Mbowe amesema, kiongozi wa mwisho wa Taifa hilo ni Hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Mbowe ambaye ni mshtakiwa wa nne katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Rushwa na Uhujumu Uchumi jijini Dar es Salaam, hajamtaja kwa jina Mwalimu Nyerere lakini ameonesha kitabu cha mwasisi huyo wa Tanzania.

Kitabu hicho, kinaelezea maisha ya Mwalimu Nyerere kilichoandikwa na Maprofesa Issa Shivji, Saida Yahya-Othman na Dk. Ng’wanza Kamata

Ni leo Jumatano, tarehe 20 Oktoba 2021, mara baada ya kuingia chumba cha mahakama akitanguliwa na washtakiwa wenzake, ameingia akiwa ameshika kitabu.


 
Mara baada ya kuingia na kukaa, akasima kuwasalimia watu waliokuwa mahakamani kisha baada ya kukaa, akachukua kitabu hicho na kukionesha juu huku akisema “kiongozi wa mwisho Tanzania huyu hapa” wengine.


Wakati Mbowe akisema Mwalimu Nyerere aliyeongoza Tanganyika na baadaye Tanzania, aling’atuka madarakani mwaka 1985 na hadi sasa, Tanzania imeongozwa na Marais watano.

Ali Hassan Mwinyi (1985-1995), Hayati Benjamin Willium Mkapa (1995-2005), Jakaya Mrisho Kikwete (2005-2015), Hayati John Pombe Magufuli (Novemba 2015- Machi 2021) na sasa Rais ni Samia Suluhu Hassan.


Mbali na Mbowe, watuhumiwa wengine katika kesi ya msingi ya uhujumi uchumi yenye mashtaka ya kula njama za kufanya vitendo vya ugaidi ni, Adam Kasekwa, Halfan Hassan Bwire na Mohammed Abdillah Ling’wenya.

Kesi hiyo inaendelea kwa Jaji Kiongozi Mustapha Siyani anasoma uamuzi wa kesi ndogo ndani ya kesi kubwa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad