Mbowe Anavyovuna Fikra Chanya Akiwa Mahabusu..Maana ya Kitabu Anachokibeba Kila Siku Mahakamani




NOMAN Vincent Peale, alikuwa mwanathilojia na mhubiri wa Injili aliyetimiza wajibu wake ipasavyo Karne ya 20. Desemba 24, 1993, alifariki dunia akiwa na umri wa miaka 95. Hakufa na kuondoka. Aliacha fikra zinazoishi.

Ni fikra hizo ndizo zinamfanya Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ajipambanue nazo, akitaka jumuiya ya Watanzania na duniani kote kuamini kwamba yupo imara na hatafsiri kilichopo kwa chuki. Hapa najaribu kucheza na ubongo wa Mbowe kwa lugha ya picha.

Mwaka 1952, Peale alitoa kitabu kinachoitwa “The Power of Positive Thinking” – “Nguvu ya Fikra Chanya”. Shabaha iliyopo kwenye maudhui ya kitabu hicho ni kuwajenga watu kuishinda mitazamo ya hofu na kuwaelekeza kuwa na imani isiyotetereka, kwamba Mungu yupo na ndiye mwenye udhibiti wa mwisho katika kila nyakati.

“The Power of Positive Thinking” kilichapwa miaka tisa kabla Mbowe hajazaliwa. Amekua na kukisoma. Bila shaka anakiamini. Anazithamini fikra za Peale. Kipindi hiki akiwa mahabusu na safari nyingi za mahakamani, akikabiliwa na mashitaka ya ugaidi, mara nyingi hupigwa picha akiwa ameshikilia kitabu hicho; Nguvu ya Fikra Chanya!

Mbowe, huingia na kitabu hicho mahakamani na hutoka nacho. Utamwona akikiweka vizuri ili wanahabari wapigapicha wakichukue na maandishi ya kwenye jalada yasomeke. Anapokaribia basi la magereza tayari kwa safari ya kuendelea na maisha ya mahabusu, hukiweka kitabu hicho kwapani, mkono mmoja akisalimia wafuasi wake kwa alama ya “vema" (salamu ya Chadema), kisha huingia garini.

MBOWE ANATAKA DUNIA IELEWE NINI?

Tuchambue lugha ya picha; kitabu cha “The Power of Positive Thinking”, Peale anaanza sura ya kwanza kwa kueleza kanuni 10 za kukabili mitazamo ya hofu na kubaki mwenye imani na Mungu. Namba moja anasema, “Jijengee picha ya kushinda kila siku". Kwamba mitihani ya dunia na hofu, visikufanye upoteze ari ya ushindi.
Kanuni ya pili ni “Fikiri kwa fikra chanya hadi fikra hasi zitoweke". tatu ni “Kupunguza vikwazo", nne “Usijaribu kuiga wengine", tano “Rudia maneno ‘kama Mungu yupo nasi, nani anaweza kushindana nasi?’ rudia maneno hayo mara 10 kila siku."


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad