Kutokana na changamoto kubwa ya maji katika jimbo la Kyela,mbunge wa jimbo hilo Ally Mlaghila Jumbe amesema jitihada zimeanza kuonekana na kuzaa matunda licha ya baadhi ya watu kudai ndoto hiyo haitakaa kutokea Kyela kupata maji.
Aidha mbunge huyo amesema haoni shida kujishusha kwa ajili ya kuwaletea maendeleo wananchi huku akiahidi kushirikiana na Serikali,Wananchi pamoja na mkuu wa wilaya kuleta huduma ya maji safi na salama Kyela na kwenye hili nipo tayari hata kubrashi viatu vya mkuu wa wilaya ilitu wananchi wangu wapate maji.
Ally Mlaghila Jumbe amesema hayo wakati akitoa maoni yake kwenye kikao acha mradi wa Maji wa 4.7 Bilioni ambao unafadhiliwa na Serikali ya Tanzania ambapo unatekelezwa na K-KAWSSA utahudumia kata 14 na kunufaisha wananchi 67,701 pindi utakapokamilika sawa na 54%