Mchungaji Aliyekataza Waumini Kutumia ARV’s Wakafariki Aomba Radhi




MHUNGAJI wa Kanisa la Evangelistic Assemblies of God Tanzania (EAGT) wilayani Rungwe mkoani Mbeya, Emmanuel Mlundilwa amesema kukosa uelewa wa kutosha juu ya matumizi ya dawa za kufubaza Virusi Vya Ukimwi (ARV’s) kulisababisha kuwakataza waumini wake kutumia dawa hizo na wakazidi kudhoofu na kupoteza maisha.

Kutokana na hali hiyo, Mchungaji huyo amewaomba radhi ndugu, jamaa na marafiki waliopoteza wapendwa wao kutokana na kutofuata ushauri wa wataalamu wa afya kutokana na msimamo wake wa kuamini wataponywa kwa maombi kutoka kwake.

Ameyasema hayo alipokuwa akitoa ushuhuda kwenye mkutano wa kuhitimisha mradi wa mapambano dhidi ya maambukizi mapya ya VVU.

Sambamba na kukomesha ukatili kwa vijana na watoto wa Pepfer FBO Initiative uliokuwa ukiendeshwa wilayani Rungwe na shirika lisilo la kiserikali la World Vision Tanzania.


 
Amesema, kupitia vifungu kadhaa vilivyopo kwenye Biblia alikuwa akiwakataza waumini waliokuwa na maambukizi ya VVU wasitumie ARV’s.

Mchungaji huyo aliwataka wategemee maombi aliyokuwa akiwafanyia mpaka alipokutana na waratibu wa mradi wa Pepfer FBO Initiative aliosema walichukua muda mwingi kumbadilisha.

Pia, amesema hadi anafikiwa na mradi huo alikuwa na waumini 15 waliokuwa wakiishi na maambukizi ya VVU na alikuwa amewaachisha kutumia dawa na wanne kati yao walikuwa taabani huku watatu wakiwa tayari wamefariki.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad