Mfano wa sahani ya chakula kupandishwa mlima Kilimanjaro





Serikali imekusudia kupandisha mfano wa sahani yenye muonekano wa mlo bora katika mlima Kilimanjaro ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha wananchi kula mlo kamili na kushiriki kikamilifu katika usindikaji wa mazao.


Kauli hiyo imetolewa leo Jumamosi Oktoba 2, 2021 na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Stephen Kagaigai, alipokuwa akitoa taarifa  kwa vyombo vya habari juu ya maadhisho ya siku ya chakula duniani yatakwayofanyika sambamba na maonyesho ya kilimo, uhifadhi wa mazingira na usindikaji wa vyakula.



Kagaigai amesema Serikali inalenga kuhamasisha wananchi kula mlo kamili kwa afya, kula vyakula vya asili na upandaji wa miti ya matunda kwa ajili ya kuboresha na kuhifadhi mazingira.



"Katika kuadhimisha siku hiyo ambayo kitaifa itafanyika mkoani Kilimanjaro, kuanzia Oktoba 10-16, moja ya vitu ambayo vitafanyika ni kupandisha mfano wa sahani yenye chakula bora katika kilele cha mlima Kilimanjaro lengo letu ni kuhasisha wananchi wote nchini kuona umuhimu wa kula vyakula bora"amesema Kigaigai



Katika hatua nyingine amesema katika maadhimisho hayo utafanyika uhamasishaji wa unywaji wa maziwa kwa wanafunzi wa shule zilizopo mkoani Kilimanjaro.



"Wananchi wajitokeze kwa wingi kuanzia siku ya uzinduzi mpaka kilele chake kwa ajili ya kuzunguka mabanda na kujifunza mambo yanayohusiana na chakula kuanzia uzalishaji hadi ulaji unaozingatia lishe bora."amesema Kagaigai
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad