Mfanyabiashara mashuhuri wa dawa za kulevya aliyekuwa akisakwa nchini Colombia na kiongozi wa genge kubwa la uhalifu nchini humo Dairo Antonio Úsuga, amekamatwa.
Úsuga, anayejulikana kama Otoniel, alikamatwa baada ya operesheni ya pamoja na jeshi, jeshi la anga na polisi siku ya Jumamosi.
Serikali ilikuwa imetoa zawadi nono ya $ 800,000 (£ 582,000) kwa yoyote ambaye anafahamu mahali alipo, huku Marekani ikiweka dau la dola milioni 5.
Rais Iván Duque amepongeza kukamatwa kwa Otoniel katika ujumbe wa video uliorushwa kwenye runinga ya Taifa.
“Huu ni ushindi mkubwa dhidi ya biashara ya dawa za kulevya katika nchi yetu kwenye karne hii,” alisema. ” Ushinid huu unafananishwa tu na anguko la Pablo Escobar miaka ya 1990.”
Otoniel alikamatwa katika maficho kwenye vijiji vya mkoa wa Antioquia kaskazini magharibi mwa Colombia, karibu na mpaka na Panama. Wakati maelezo ya operesheni bado yakiibuka, rais amesema afisa mmoja wa polisi aliuwawa kwenye majibizano ya risasi. a
Wanajeshi wa Colombia walitoa picha inayoonyesha wanajeshi wake wakimzingira Otoniel aliyefungwa pingu.