Mkusanyiko nadra wa kazi za michoro ya mwanamasumbwi gwiji Muhammad Ali imeuzwa kwenye mnada kwa karibu dola milioni 1 (£733,760) swa na Tsh 2,307,000,000/=
Kazi zake 26 za usanii zilipelekwa katika jumba la mnada la Bonhams mjini New York.Mojawapo ya kazi zilizosubiriwa ni ule wa mfano wa nyuki, uliouzwa kwa dola 425,000 (£311,853), sawa na Tsh 980,475,000/= kiasi hicho kikiwa ni mara 10 ya makadirio ya awali ya mauzo yake.
Ali alisifiwa kwa kuwa mmoja wa wanariadha bora zaidi, mwanaharakati na mshairi, lakini usanii wake wa kuchora haukujulikana.
Kituo cha manada cha Bonhams kilisema alichora katika maisha yake –akitiwa moyo na baba yake ambaye alikuwa mchoraji aliyesomea taaluma hiyo na hatimaye alifanya masomo kutoka kwa msanii wa michezo LeRoy Neiman.