Mji wa Uingereza kuhifadhi sanamu ya mvumbuzi wa Afrika





Sanamu ya mtu aliyevumbua Afrika HM Stanley itaendelea kuhifadhiwa katika mji wa kaskazini mwa Uingereza wa Wales, baada ya kura iliyopigwa na watu katika eneo hilo.
Wakazi wa Denbigh ambao walishiriki katika kupiga kura wote walipiga wingi wa kura kuhifadhiwa kwa sanamu hiyo ya shaba ya Stanley, ambaye alizaliwa katika mji huo.

Kura ya mashauriano iliitishwa ili kuondoa sanamu hiyo ya Stanley kufuatia madai kwamba alifanya ukatili na ubaguzi wakati wa uvunduzi wake.

Mvumbuzi huyo ni maarufu sana kwa kuwapata wamishonari, akisema maneno : "Dkt Livingstone, ninadhani?"

Stanley alimtafuta na kumpata Dkt David Livingstone katika eneo lisiloweza kufikiwa kwa urahisi la sehemu ambayo sasa inaitwa Tanzania katika mwaka 1871.

 

OPEN IN BROWSER

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad