Mkosoaji wa Rais Kagame Ahukumiwa Miaka 15 Jela



Mkosoaji wa Utawala wa Rais Paul Kagame aliyejizolea umaarufu mkubwa kutokana na video zake kupitia #YouTube amehukumiwa miaka 15 jela Mjini Kigali

Yvonne Idamange (42) amekutwa na makosa sita ikiwa ni pamoja na uchochezi wa ghasia na uasi, kupuuza kumbukumbu za mauaji ya kimbari, kueneza habari za uzushi na kuchochea vurugu

Kupitia YouTube, Idamange alimshtumu Rais Kagame na Serikali yake kwa kuanzisha udikteta, kutumia mauaji ya kimbari ya 1994 kwa maslahi yao bila kuwapa msaada wowote wahanga na kugeuza eneo la kumbukumbu ya mauaji hayo kuwa kivutio cha Utalii.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad