Tirop, ambaye alipatikana ameuawa nyumbani kwake Iten, alikuwa anaishi na Ibrahim Rotich lakini ndoa yao ilikuwa na doa.
Kulingana na Kamanda wa Polisi wa Keiyo North, Tom Makori, baba yake Tirop jioni ya Jumanne, Oktoba 12, alipiga ripoti kuwa mwanariada huyo ametoweka.
Siku ya Jumatano, Oktoba 13 mwendo wa saa tatu asubuhi, Makori alisema Rotich anaripotiwa kuwapigia wazazi wake simu na kuwafahamisha kuwa ndiye alitenda kitendo hicho chaa kinyama na kumuomba Mwenyezi Mungu msamaha.
Baada ya simu hiyo, familia ya marehemu na majirani walikimbia nyumbani kwake na kupata mwili wake umelowa damu kitandani.
Mwili wa Tirop ulikuwa na majeraha ya kisu tumboni.
Duru ilidokezea kuwa Tirop alikuwa na mvutano na mume wake na kupigana kila mara.
Wawil hao wanaripotiwa kupatanishwa mara kadhaa na familia na marafiki.
Majirani walisema marehemu alirejea kwa mume wake Jumatatu, Oktiba 11, kufuatia kuondoka wiki kadhaa baada yao kutofautiana.
"Hajakuwa nyumbani tangu arejee kutokea Japan. Tirop alisema alipigwa na kutorokea katika kambi ya mazoezi kutafuyta hifadhi. Alikuwa amerejea tu kwake baada ya familia na marafiki kuwapatanishi," mmoja wa majirani alisema
Polisi wanamsaka Rotich ambaye ni mshukiwa mkuu wa mauaji ya Tirop. Alihepa baada ya kisa hicho.
Hatua za mwisho za Tirop
Picha ambazo iliziona zilionyesha wapenzi hao wawili wakifurahia wakati mzuri pamoja na kwa hivyo wanapendana.
Iliripotiwa kwamba huu ndio ulikuwa wakati wake wa mwisho mikoni mwa mpenzi wake Kipleting.
Agnes Tirop: Rais Uhuru Aamuru Polisi Kuharakisha Uchunguzi wa Mauaji ya Mwanariadha
Katika picha hiyo, dada huyo mwenye umri wa miaka 25 alikuwa amekumbatiwa na mpenziwe huku wawili hao wakionekana kuwa na furaha.
Hata hivyo inadaiwa dada huyo alipoteza maisha yake kutokana na majeraha aliyosababishiwa na mpenzi wake penzi lao lilipoingia doa.
Mshikilizi wa rekodi ya dunia
Mnamo Septemba 12, 2021, marehemu alivunja rekodi ya wanawake ya kilomita 10 ambayo ilishikiliwa na Asmae Leghzaoui wa Morrocco.
Katika Olimpiki za Tokyo za 2020, Tirop aliibuka wa nne katika fainali za wanawake za mita 5,000 baada ya kutumia muda wa 14: 39.62.
Katika mbio hizo, Sifan Hassan wa Uholanzi aliibuka mshindi baada ya kutumia muda wa 14: 36.79.
Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 25, mnamo 2019, alishinda shaba katika mbio za mita 5000.
Mnamo mwaka wa 2015, alishinda tuzo za Mashindano ya Cross Country Championships.