Muziki wa Nigeria Umeipiga Sana Bao Bongo Flava..Kazi Yetu Kushindanisha Mondi na Harmonize Nani Kajaza


Inasikitisha sana, hivi sasa sio tu muziki wa nigeria umetukimbiza kimataifa bali unakimbiza mpaka kitaifa, yani ndani humu ya Tanzania muziki wa Nigeria umebamba kila kona.

Hivi sasa katika watanzania 10 basi nane lazima wawe na ngoma za Wizkid, Burnaboy, Plus hawa Vijana ambao kwasasa ni moto wa kuotea mbali, Omah lay, Joe Boy, Rema, simi, Ruger, Chike, nakadharika.

Sio kwenye simu za watu tu, bali hata redio na Tv za Tanzania, zinapiga sana nyimbo za Nigeria, Club kidogo zimepungua , maana kwasasa Amapiano zimetawala pande hizo.

Ukisikiliza Top twenty za Redio nyingi mfano Jumapili hii Kwenye kipindi cha Top Twenty Cloudsfm utaona nyimbo za naigeria zinafanya poa sana.

Hii support tunayowapa tungewapa wasanii wa ndani, leo hii wangefika mbali, tatizo ni nini? ni kwamba nigeria wanatushinda sana kuimba, mpaka tunapendezwa na ngoma zao kuliko za hapa Tanzania? Maana kuna ngoma kama "medicine" "Sip(Alcohol)" "Essence" zinatrend sana Tanzania kuliko hata Za humu humu.

Kazi yetu ni kushindanisha tu harmonize na Mond nani kajaza watu kwenye show. Imagine amapiano Imebamba Tanzania, Muziki wa Nigeria Umebamba Tanzania, hivi wasanii wetu wamelala au Wameshaumaliza mwendo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad