KWA kawaida tumezoea kuona ama kusikia mwanamke akijifungua mtoto mmoja, mapaha wawili na mara chache sana mapacha watatu au wanne, ni nadra sana mwanamke kuzaa watoto zaidi ya watatu.
Lakini hii ya leo imekuwa ya tofauti kidogo, mwanamke mmoja amejifungua watoto saba katika Mji wa Abbottabad nchini Pakistan na watoto wote pamoja na mama yao wapo salama.
Mume wa mwanamke huyo, aitwaye Yar Mohammed anasema uchunguzi wa awali ulipobaini mke wake amebeba watoto kadhaa tumboni walishauriwa waende hospitali kuu kwa uangaalizi wa karibu.
Daktari bingwa wa wanawake katika Hospitali ya Jinnah mjini Abbottabad, Dk. Hina Fayaz, , mwanamke huyo alifika Hospitali hapo kwa mara ya kwanza Jumamosi iliyopita. “Baada ya uchunguzi wa ultrasound na ripoti zingine, tuligundua kuwa ana watoto watano ndani ya tumbo lake na ujauzito wake ulikua zaidi ya miezi minane.”
Dk. Hina Fayaz anasema kwamba alishtuka sana kuona ripoti ya matibabu ya mwanamke huyo. Madaktari waliomhudumia walishangazwa sana na hali ya mwanamke huyo.
“Alikuwa na shinikizo la damu iliyotajwa kuwa ya kiwango hatari. Tumbo lake lilikuwa limevimba. Kabla ya hapo, alikuwa amejifungua na watoto wawili kwa nja ya upasuaji. Alikuwa na maumivu makali kwenye kovu la upasuaji wa kwanza.”
“Hata hivyo madaktari walifanikiwa kuwatenganisha watoto hao kabla ya kuwatoa tumboni. Tulijitahidi sana kuhakikisha mama asipoteze damu nyingi wakati wa kuwatenganisha.”
Watoto hao kwa sasa wanapewa uangalizi maalum ambapo baba yao anasema kuwatunza haitakuwa kazi ngumu kwa sababu anaishi na jamaa zake. “Mungu ametujaalia watoto wanne wa kiume na watatu wa kike. Tunafuraha sana, lakini itakuwa ngumu kwetu kuwatunza kulingana na hali ya maisha yetu,” alisema Mohammad.