Mwananchi, Wasafi , TBC na Clouds waungana maadhimisho ya uhuru

 


Dar es Salaam. Mkataba wa ushirikiano wa vyombo vinne vya habari kuadhimisha miaka 60 ya uhuru umebeba malengo saba ya kuileta Tanzania pamoja.

Hayo yamesemwa leo Jumanne Oktoba 26, 2021 na mwakilishi wa Mkurugenzi wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), Gabriel Nderumaki kwenye uzinduzi wa nembo itakayotumika katika maadhimisho ya miaka 60 ya uhuru na kusaini mkataba wa ushirikiano baina ya Mwananchi Communications Limited, Wasafi Tv, TBC na Clouds Media.

Amesema  vyombo hivyo vimekaa pamoja  na kuona ni muda sahihi wa kuwaunganisha Watanzania kuhamasisha uzalendo na kuangalia changamoto na fursa zilizopo.

“Lengo ni kuangalia mustakabali wa nchi yetu, tulipotoka, tulipo na tunapokwenda. Mchango wa wananchi,  kutoa tuzo kwa viongozi waliofanya vizuri, kukuza utamaduni  kama tunavyofahamu mmomonyoko wa maadili ulivyo kwa sasa,” amesema Nderumaki.

Vyombo vya habari amesema vina lengo la kukuza maendeleo, kukusanya taarifa za uchumi wa nchi yetu  na kuwafikia wananchi wengi zaidi.

“Dhima yetu ni kuwaleta wananchi pamoja. Vijana wengi hawajui kuhusu uhuru wa nchi yao hivyo muunganiko huu utasaidia kutoa elimu sahihi kwa vijana,” amesema Nderumaki.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad