Web

Mwanzilishi wa bomu la nyuklia, Pakistan afariki kwa Corona




Mtu anayechukuliwa kama “mwanzilishi wa bomu la nyuklia la Pakistan”, Dk Abdul Qadeer Khan, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 85 baada ya kuugua ugonjwa wa Covid-19.

Abdul Qadeer Khan: ′Father′ of Pakistan′s atomic bomb dies at 85 | News |  DW | 10.10.2021

Dr Khan alisifiwa akiitwa shujaa wa kitaifa kwa kuibadilisha nchi yake kuwa taifa la kwanza la kiislamu lenye nguvu za nyuklia ulimwenguni.

Lakini pia alikuwa maarufu kwa kupenyeza magendo ya siri za nyuklia kwenda nchi nyingine zikiwemo Korea Kaskazini na Iran.

Waziri Mkuu Imran Khan alisema Pakistan imepoteza “mtu muhimu”. Alipendwa na taifa letu kwa sababu ya mchango wake muhimu katika kutufanya kuwa taifa la silaha za nyuklia,” Waziri Mkuu aliandika kwenye ukurasa wa twitter

Anajulikana kama AQ Khan, mwanasayansi huyo alisaidia sana kuanzisha kinu cha kwanza cha urutubishaji wa nyuklia huko Kahuta karibu na Islamabad nchini Pakistani. Kufikia 1998, nchi hiyo ilikuwa imefanya majaribio yake ya kwanza ya nyuklia.

Lilikuwa muda mfupi baada ya majaribio kama hayo kufanywa na India, kazi ya Dr Khan ilifanya Pakistan kuwa nchi ya saba kuwa na nguvu za nyuklia ulimwenguni na kusababisha shangwe kitaifa.

Lakini alikamatwa mwaka 2004 kwa kushiriki teknolojia ya nyuklia kinyume cha sheria na Iran, Libya na Korea Kaskazini.

Ripoti zilizobainisha kuwa alipeleka siri za nyuklia kwa nchi nyingine ziliishtua Pakistan.

Katika hotuba kwa njia ya televisheni, Dk Khan aliomba msamaha kwa “majuto makubwa”.

Dk Khan alisamehewa na rais wa wakati huo wa Pakistan, Pervez Musharraf, lakini alikuwa chini ya kizuizi cha nyumbani hadi mwaka 2009.

Kushikiliwa kwake kuliwakasirisha wengi hasa mataifa ya magharibi, ambapo alipewa jina la “msambazaji mkubwa wa teknolojia ya nyuklia wa wakati wote”.

Lakini huko Pakistan alibaki kuwa ishara ya kujivunia kwa jukumu lake katika kuongeza usalama wa kitaifa.

“Alitusaidia kukuza kinga ya taifa na taifa lenye shukrani halitasahau huduma zake,” Rais Arif Alvi alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad