KUELEKEA kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC, Kocha Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi, ameandaa
dozi nzito ambapo amewapa wachezaji wake mazoezi maalum ya kufanya kuanzia jana na leo.
Mchezo huo wa ligi kuu unatarajiwa kupigwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar huku Yanga
wakiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wao wa mwisho dhidi ya Azam kwenye uwanja huo kwa msimu
uliopita.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli, alisema: “Kila kitu kinaenda
sawa kuelekea kwenye mchezo wetu wa ligi dhidi ya Azam, wachezaji wote wapo fiti.
“Nabi anasema watu wategemee mabadiliko makubwa kwenye uchezaji lakini wasitarajie mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha kwanza kwani timu inayokupa ushindi huwezi kubadilisha.
“Timu wiki hii imekuwa na program tofauti tofauti kwani Jumatatu mpaka Jumatano walifanya mazoezi mara mbili huku leo Alhamisi wanafanya mazoezi mara moja tu hata kwa siku ya kesho Ijumaa.
Stori: Leen Essau, Dar es Salaam