Ndoto za Ndugai kuwa Hakimu zilivyozimwa Kibaha




Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema hapo awali alitamani kuwa Hakimu wa Mahakama ya mwanzo  lakini ndoto hiyo ilizimwa na Mkuu wake wa Shule ya Kibaha miaka hiyo akiwa kidato cha tatu.


Spika Ndugai
Ndugai ameyasema hayo leo wakati wa uzinduzi wa Jengo la Mahaka ya Mwanzo ya Kibaigwa ambapo ameweka wazi wakati wa kupangiwa michepuo kidato cha tatu alitaka apelekwe darasa la watu wa Arts’ lakini akaambiwa aende Sayansi.

Ndugai anasema lakini hajisikii vibaya kwa kukosa nafasi ile kwani hata sasajapo siyo Hakimu lakini anafurahia kuwa katika sehemu ya watunga Sheria za nchi.

“Baba yangu alikuwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo sehemu nyingi sana ikiwa ni pamoja kule Ukerewe. Kuna wakati nilikuwa natamani kuwa Hakimu na mimi. Lakini wakati ule tunapangwa kwenda kwenye michepuo nakumbuka ilikua kidato cha tatu, Mkuu wangu wa shule miaka hiyo Kibaha Sekondari akaniambia  unataka kuwa Binaisa (Rais wa zamani wa Uganda). Akanifukuza ofisini kwake na  kwenda Sayansi kule kwa kina Ole Gabriel nikaishia kuchunga ng’ombe. Nayo ni maisha sijawa mtafsiri sheria, nimekua mtunga sheria siyo mbaya sana,“Spika Ndugai.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad