Wanaijeria waandamana wakimtaka Rais Buhari ajiuzulu




Kumekuwa na maandamano katika mji mkuu wa Nigeria, Abuja wakiwa wamebeba mabango yanayomtaka Buhari kuachia madaraka #BuhariMustGo.
Maandamano hayo yamefanyika katika siku ya madhimisho ya uhuru.

Polisi waliwatawanya waandamanaji hao kwa kufyatua mabomu ya gesi.

Haijawekwa wazi kama kuna yeyote aliyekamatwa kufuatiwa maandamano hayo.

Mwanaharakati wa Haki za binadamu Omoyele Sowore aliwataka raia wa Nigeria kuandamana nchi nzima katika siku ya uhuru wa nchi hiyo.

Katika hotuba ya Rais Muhammadu Buhari katika siku ya uhuru haikutoa msisitizo changamoto za kiusalama katika taifa hilo na kushuka thamani kwa fedha ya Nigeria yaani Naira.

Hivyo suala la kupuuzia kutekwa kwa wanafunzi zaidi ya 1,000 kaskazini mashariki mwa nchi hiyo , Rais Buhari alisema vyombo vya usalama nchini Nigeria zinafanya kubwa na karibu tunafanikiwa katika hilo.

Kwenye kurasa ya Twitter baadhi ya watu wanaandika juu ya sherehe za uhuru wakati wengi wakiikosoa serikali

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad