Nyayo za Binadamu wa ‘Kale Zaidi’ Aliyeishi Miaka 23,000 Zapatkana




MATOKEO ya hivi karibuni ya ugunduzi katika juhudi za kutafuta binadamu walioishi kabla ya historia kuanza kuandikwa ambao waliishi miaka 21,000 hadi 23,000 yamevunja rekodi ya makadirio ya awali ya uwepo wa binadamu wa kwanza katika Bara la Amerika.

 

Mada kuhusu ni lini binadamu wa kwanza walikanyaga katika ardhi ya Marekani kutoka Asia imekuwa yenye utata kwa miongo kadhaa. Wanasayansi wengi wana wasiwasi na Ushahidi uliopo unaosema kuwa binadamu wa kwanza kufika ndani ya Amerika ya Kaskazini zaidi ya mika 16,000 iliyopita.

 

Sasa, jopo la wanasayansi wanaofanya kazi katika New Mexico wamebaini nyayo za binadamu kadhaa ambazo zinakadiriwa kudumu baina ya miaka 21,000 hadi 23,000. Matokeo ya utafiti huu yanaweza kubadili mtazamo wa ni lini bara la Amerika lilikaliwa na binadamu kwa mara ya kwanza.

 

Matokeo haya pia yanaelezea uwezekano wa kuhama kwa idadi kubwa ambayo bado haujajulikana. Na hii inaibua uwezekano kwamba watu hawa wa kale walikuja kutoweka. Nyayo hizi zimejitengeneza katika matope laini kwenye mwambao wa ziwa dogo ambalo kwa sasa ni sehemu ya ziwa kavu tambarale la Alkali lililopo katika mbuga ya wanyama ya kitaifa ya White Sands.

 

Wanasayansi kutoka Taasisi ya utafiti wa kijiolojia ya Marekani walifanya uchunguzi huu kwa kutumia kifaa radiocarbon kinachochunguza (sampuli) za mazao yaliyopatika kwenye tabaka za juu na chini za mahali ambapo nyayo hizo zilipatikana.




Kutoka pale, watafiti hao waliweza kupata tarehe halisi ambayo nyayo hizo ziliachwa. Kutokana na ukubwa wa nyayo hizo, watafiti wanasema, upenyo huo ulipitiwa kwa mara ya kwanza na migu ya vijana wenye umri wa kubalehe na watoto wadogo waliokuwa wakisafiri kwenda na kurudi- wakati mwingine wakiambatana na watu wazima.

 

Watafiti walibaini umri wa nafaka zilizokuwa juu na chini ya tabaka za nyayo za binadamu walioishi kabla ya historia. Matokeo haya yamefungua dirisha jipya la kusisimua katika kutaka kujua maisha yalivyokuwa kwa wakazi wa kale walioishi katika eno ambalo sasa ni la Kusini magharibi mwa Marekani.

 

Ushahidi wa nyayo sio kama jiwe
Watafiti hawajui kusema kweli ni nini hasa walichokuwa wakikifanya vijana hao, lakini inawezekana kuwa walikuwa wanawasaidia watu wazima kuwinda. Hii ilionekana baadaye miongoni mwa tamaduni za wazawa wa Marekani.

 

Uwindaji huu wa wanyama unafahamika kama buffalo jump.

Mchezo wa Wanyama “hufanyika kwa muda,”anaelezea Dkt Sally Reynolds, mwandishi mwenza katika Chuo kiku cha Bournemouth.

 

Zana za sanaa zilizotumiwa wakazi wa zamani mara nyingi huwa hazieleweki kwa urahisi na ni ngumu kuzielewa kuliko zile zilizotengenezwa kwa ncha za mikuki katika Amerika Kaskazini miaka 13,000 na zaidi. Hii inaibua wasiwasi kuhusu utambulisho wake halisi.

 

“Mojawapo ya sababu kuna mjadala mkubwa ni kwasababu ya ukosefu wa data halisi. Hiyo ndio maana tulifikiri, kuna uwezekano mkubwa tulipata matokeo halisi ,”, alisema Profesa Matthew Bennett, Mwandishi mkuu wa utafiti huu katika jarida la utafiti la chuo kikuu cha Bournemouth.

 

Jiwe lililotengenezwa na watu wa jamii ya Clovis. Linaaminiwa kuwa na muonekano wa mwanadamu wa mwanzo kabisa aliyeishi Marekani

 

“Nyayo sio sawa na jiwe lililochorwa kwa usanii. Nyayo ni nyayo , na hizi haziwezi kusonga juu wala chini [ katika ufongo mdogo ].”

 

Huku asili ya ikiwa ni vigumu kupuuza ushahidi huu wa mwili, watafiti watatakiwa kuhakikisha ushahidi wa tarehe ni halisi.

 

Suala gumu ambalo lilibainiwa na jarida wakati wa hatua za mwanzo za utafiti lilikuwa ni ”athari za hifadhi”. Hii inamaanisha kutunzwa wakati mwingine kwa kipimo cha kaboni katika mazingira ambayo yanaweza kubadili uasili kutokana na hali iliyopo ya kimazingira, kwa kufanya eneo kuonekana kuwa la miaka mingi kuliko umri wake.



Hata hivyo watafiti walisema kuwa walikuwa wamezingatia kwa umakini athari hii , na wanaamini ilikuwa na athari ndogo sana kwa jiwe walilolifanyia utafiti.

 

Profesa Tom Higham, mtaalamu wa utambuzi wa kipimo cha umri cha radiocarbon katika Chuo kikuu cha Vienna alisema : “Walipatia umri vitu vilivyokuwa kando ya eneo zilikopatikana nyayo , na kubaini kuwa sampuli za mkaa (zilionyesha umri sawa na spishi ambao waliwapima karibu na eneo zilipokuwa nyayo za miguu.

 

Katika nusu ya pili ya karne ya 20 , wanaakiolojia wa Marekani waliafikiana kuwa watu wa jamii ya Clovis walikuwa wa kwanza kufika Amrika.

 

Clovis ni watu waliokuwa na utamaduni wa Palaeo-na Wahindi katika amerika ya kati na kaskazini ambao wanakadiriwa kuishi miaka 11,500 – 11,000 iliyopita ambao waliacha jiwe lenye ncha ya mkuki linalofahamika kama ncha za Clovis.


Watafiti walikichunguza matabaka ya mchanga

Wimbi hili la binadamu walioishi katika kipindi cha kabla ya kuandikwa kwa historia ya binadamu linadhaniwa kuwa lilivuka daraja la ardhi linalopita Bering Strait na kuunganisha maeneo ya Siberia na Alaska wakati wa zama za mwisho za barafu , wakati viwango vya bahari viliposuka.

 

Wakati wazo la “Clovis wa kwanza ” lilipojitokeza, ripoti za wakazi wa kare zilionekana kuwa sio za kuaminika, na baadhi ya wanaakiolojia waliamua kuacha kutafuta tena dalili za watu walioishi zama za kale katika Amerika. Lakini katika miaka ya 1970 mtizamo huu wa kizamani ulibadiliswa.

 

Kufikai miaka ya 1980, ushahidi imara wa uwepo wa binadamu aliyeishi miaka 14,500 ulikuwa umejitokeza katika eneo la Monte Verde nchini Chile.

 

Na tangu miaka ya 2000, maeneo mengine ya kabla ya eni ya Clovis yamekuwa yakikubaliwa na wengi-kama vile eneo alipoishi mgiriki miaka 15,500- la Buttermilk Creek Complex lililopo Texas, na Eneo la Cooper Ferry aliyeishi miaka 16,000- katika Idaho.

 

Sasa, ushahidi kutoka New Mexico sunaonyesha binadamu alikuwa amekanyaga mguu wake ndani ya Amerika Kaskazini katika mwisho wa Zama za Barafu. Gary Haynes, profesa katika chuo kikuu cha Nevada, Reno, alisema: ” Sioni kasoro yoyote katika matokeo ya utafiti au fasili yake – jarida hili ni muhimu na lenye kuchochea.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad