Nyota Simba Aipa Ubingwa Yanga SC





NYOTA wa zamani wa klabu ya Simba raia wa Ghana Nicholas Gyan amesema kuwa Yanga ya msimu huu ni bora kuliko Yanga zote za misimu minne iliyopita na ina nafasi ya kutwaa ubingwa.

Gyan alisema Simba hawatakiwi kubweteka badala yake wawe makini kwa kuwa mwenendo wa Yanga ya msimu huu unaonekana bora sana na kila mchezo wanaocheza wanaonekana kubadilika na kuwa bora zaidi.

Gyan ambaye kwa sasa yupo na kikosi cha DTB FC kinachoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, aliwahi kutwaa mataji mawili akiwa na Simba, msimu wa 2017-18 na 2018-19 kisha akatemwa baada ya kukosa nafasi ya kudumu.

Akizungumza na Championi Jumatatu Gyan alisema: “Uwa natazama mechi ya Simba na Yanga kama ambavyo imekuwa desturi ya Watanzania wengi. Yanga wanaonekana kuwa wanahitaji kitu msimu huu.

“Na kwa namna ambavyo walivyo bora naona wanakwenda kufanya mambo makubwa sana, siyo Yanga ile ya misimu minne nyuma, hii iko bora zaidi na Simba wanatakiwa kuwa makini zaidi kwa kuwa mwisho wanaweza kutoka kapa.”

 

ISSA LIPONDA, Dar es Salaam

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad