Paula Hataki Kumkosa Rayvanny





MREMBO Paula Paul almaarufu Paula Kajala; mpenzi wa staa wa Bongo Fleva, Raymond Mwakyusa au Rayvanny anaamini kwamba, riziki ni riziki tu kama Mungu amempangia binadamu na maisha hayampi mtu kitu bora mara mbili isipokuwa hutokea mara moja tu kama ilivyotokea kwake kumpata Rayvanny.

 

Kauli hiyo ya Paula ameitoa wakati huu akiwa masomoni nchini Uturuki huku nyuma nchini Tanzania kukiwa na mambo mengi yanayozungumzwa juu ya penzi lake na Rayvanny. Kibongobongo, kwa kapo ya Paula na Rayvanny ndiyo inayozungumzwa zaidi ukilinganisha na kapo nyingine za mastaa Bongo.

 

Mara kadhaa wawili hao wamekuwa wakisifiana; kila mmoja akimwambia mwenzake anayajua mapenzi huku Rayvanny akienda mbali zaidi na kumtungia hadi wimbo Paula unaoitwa Wanaweweseka.

 

Kwa upande wake, Paula amekuwa akieleza namna ambavyo anainjoi mno penzi la Rayvanny na hawezi kumuacha au hataki siku moja jamaa huyo aondoke kwenye himaya yake na kwenda kwa mwanamke mwingine au kurudi kwa mama wa mtoto wake, Faima Msengi au Fahyma.

 

Hata hivyo, kwa upande wake, Rayvanny alishaweka wazi kuwa, kurudi kwa Fahyma ni jambo ambalo halitawezekani kabisa, badala yake ataendelea kubaki na mrembo wake huyo ambaye ni Paula.

 

Tangu ametua masomoni Uturuki, Paula amekuwa akiandika maneno matamu ya mapenzi kupitia Insta Story yake ambayo yanakwenda kwa Rayvanny au Chui, akieleza ni kwa namna gani anampenda kiasi kwamba hataki kabisa jamaa huyo aje aondoke kwenye maisha yake.

 

Moja ya jumbe hizo za Paula kwenda Rayvann, jana ulisomeka; “Take care of him, cause life doesn’t bless you with a good man twice…” Akimaanisha mjali mwanaume kwa sababu maisha hayawezi yakakubariki na mwanaume bora mara mbili au zaidi ya mara moja kwa sababu siku zote maisha yanampa mtu kitu bora mara moja tu!

 

Kwa kifupi; Paula anamaanisha kwamba amepewa Rayvanny ambaye ni mwanaume bora ambaye anamjali na ataendelea kumtunza kwa sababu ndiye wa kwake wa maisha hivyo suala la yeye kuachana na jamaa huyo watu wataendelea kulisikia kwenye bomba tu.

STORI; KHADIJA BAKARI, DAR


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad