Picha: Mabaki ya Mijusi Mikubwa Kuliko Wote Duniani Dinosaur Yapatikana Lindi


Watafiti kutoka Makumbusho ya Taifa, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Watafiti kutoka Ujerumani, wamegundua masalia mapya ya mijusi wakubwa aina ya Dinosaur walioishi miaka milioni 150 liyopita huko Lindi maeneo ya Tendaguru.

Mhifadhi na Mtafiti Mwandamizi wa Akiolojia Makumbusho ya Taifa Dkt Agnes Gidna, Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu Dar es Salaam Dkt Frank Masele na Mtafiti kutoka Makumbusho ya Naturkunde Berlin Ujerumani Dkt Daniela Schwarz wamesema huo ni utajiri mwingine wa Akiolojia uliopo Tanzania.


"Wameishi katika eneo hili miaka milioni 150 iliyopita katika utafiti wetu huu tumegundua masalia mengi pamoja ya kwamba tupo hapa kwa muda mfupi, hadi sasa pengine tuna tani 2, tumegundua mifupa ya miguu ambayo ipo kamili, tumegundua mifupa ya migongo, mbavu na masalia mengi, hii inaonesha ni dalili nzuri kwa Nchi na najivunia kuwa Mtanzania mtafiti" Dr. Agnes Gidna.

Bado masalia hayo yapo Katika eneo hilo la Tendeguru Mkoani Lindi ambako yamegunduliwa yakisubiri Mamlaka za Nchi ziamue yatafahidhiwa wapi.



Itakumbukwa Mwezi January mwaka huu iliripotiwa taarifa ya Wabunge 10 wa Bunge la Tanzania kuanzisha Kamati maalum ya kuhakikisha sehemu ya mapato ya utalii yanayotokana na mabaki ya mjusi mkubwa (Dinosaur) aliyeko katika jumba la makumbusho Ujerumani yanarejeshwa Tanzania, mabaki hayo yalivumbuliwa katika eneo la Tendegru mkoani Lindi zaidi ya miaka 100 iliyopita ambapo mabaki yalichukuliwa nchini mwaka 1905.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad