Polisi Lindi waua dereva wa lori aliyedaiwa kutaka kuwapora bunduki




Lindi. Dereva wa gari kubwa Ibrahimu Saidi (35) amefariki dunia na askari watatu wamejeruiwa na kulazwa hospital ya Mkoa Sokoine baada dereva huyo kudaiwa kumgonga askari mmoja na kudaiwa kutaka kupora bunduki.

Tukio Hilo limetokea Oktoba 17, 2021 saa 5:30 usiku kwenye kizuizi cha Polisi kilichopo maeneo ya Sido Lindi mjini.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, Mtatiro Kitinkwi amekiri kutokea kwa tukio hilo akisema askari wanne waliokuwa eneo hilo walisimamisha lori lililokuwa na tela, lililokuwa ikiendeshwa na dereva Ibrahim Said (35) likitokea Dar esaalama kuelekea Mtwara.

Alisema hata hivyo dereva huyo aliyekuwa na abiria, hakusimama na badala yake mgonga askari aliyekuwa akisimamisha gari hlo na kuacha njia na kugonga mti.


 
Alisema, baada ya hapo dereva huyo alishuka na kwenda kumvamia askari mwingine aliyekuwa na silaha na kuanza kumchoma kisu sehem mbalimbali za mwili akiwa na lengo la kumpora silaha yake.

Alisema askari huyo mwenye silaha alijihami kwa kumshambulia dereva huyo kwa risasi zilizosababisha dereva huyo afariki.

Alisema katka tukio hilo afisa mmoja na askari wawili waliumia katika mapambano hayo na wamelazwa katika hospital ya Mkoa Sokoine na afya zao zinaendelea vizuri.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad