Dube katika mchezo wao wa leo Jumamosi dhidi ya Yanga, kufuatia kutotengemea kwa afya yake na sasa anaendelea na programu maalum.
Dube hajaonekana uwanjani tangu alipougua tumbo ghafla, na kulazimika kutolewa uwanjani katika mchezo wa robo fainali ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Rhino Rangers ya Tabora, uliopigwa Mei 26, mwaka huu.
Kutokana na changamoto hiyo, Dube alifanyiwa upasuaji mdogo wa ambao ulitarajiwa kumuweka nje kwa kipindi cha miezi miwili.
Mzimbabwe huyo msimu uliopita alihusika kwenye upatikanaji wa mabao 19, akiweka kambani mabao 14 na kuasisti mabao matano.Akizungumza na Championi Jumamosi, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano wa Azam, Zakaria Thabith ‘Zaka Zakazi’ alisema: “Tunatarajia kumkosa nyota wetu Prince Dube katika mchezo wetu wa kesho (leo), Jumamosi dhidi ya Yanga kutokana na mapumziko ambayo amepewa kama sehemu ya matibabui yake.
“Sambamba na mapumziko hayo Dube amepewa programu maalum ya mazoezi kuhakikisha anarejea akiwa fiti zaidi na kwenye kasi yake ya kawaida ya kufunga kama ilivyokuwa msimu uliopita.”
NA JOEL THOMAS,Dar es Salaam