Rais Buhari ahimiza utulivu baada ya shambulio lililowaua watu zaidi ya 40 Nigeria





Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari ametuma risala za rambi rambi kwa familia za watu waliouawa katika shambulio kwenye soko la kijiji katika jimbo la kaskazini magharibi la Sokoto.

Serikali ya jimbo la Sokoto ilisema watu 43 walifariki katika shambulio la Jumapili jioni baada ya watu wenye silaha kuvamia soko la wazi katika mji wa Goronyo.

Katika taarifa yake, Rais Buhari anatoa wito kwa Wanigeria "wasikate tamaa" lakini "waendelee kuwa na subira" kwani mamlaka "zimeazimia zaidi kuliko hapo awali kuwalinda Wanigeria".

Serikali yake imekosolewa vikali kwa kushindwa kukabiliana na ukosefu wa usalama ulioenea nchini, na mauaji na utekaji nyara unaotekelezwa na vikundi vyenye silaha vinaongezeka.

Mashambulio yameendelea licha ya kupelekwa kwa maelfu ya maafisa wa vikosi vya usalama na pia kuzuiwa kwa mtandao na huduma za simu za rununu katika sehemu nyingi za kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad