Rais Kenyatta Akutana na Rais Biden, Wazungumza Mazito





RAIS Uhuru Kenyatta juzi usiku aliingia katika kitabu cha kumbukumbu kama rais wa kwanza kutoka Barani Afrika kualikwa na Rais wa Marekani, Joe Biden katika ikulu ya  White House tangu kiongozi huyo wa Marekani kuapishwa rasmi Januari mwaka huu.

 

Mkutano huo wa kihistoria na Rais  Biden, ulitangaza msaada wa serikali ya Marekani wa dozi milioni 17 zaidi za chanjo dhidi ya ugonjwa wa  Covid-19 kwa muungano wa Afrika, ambayo ni sehemu ya dozi milioni 2.8 ambazo Kenya imepokea kutoka kwa Marekani.

 

“Nina furaha kutangaza kuwa tunatoa mchango wa kihistoria wa moja kwa moja wa dozi milioni 17 za chanjo aina ya Johnson and Johnson kwa umoja wa Afrika, na tutaendelea kutoa dozi zingine kufikia mwishoni mwa mwaka huu kwa Kenya,” alisema Rais Biden.

 

Rais  Kenyatta aliishukuru serikali ya marekani kwa kuendelea kuisaidia Kenya na bara la Afrika kukabiliana na janga hilo la  Covid-19.

 

“Nachukua fursa hii kuishukuru serikali na watu wa Marekani. Wakati wa kipindi hiki kigumu, serikali ya Marekani ilijizatiti sio tu kuisaidia Kenya mbali pia bara nzima la Afrika kwa jumla katika upatikanaji wa chanjo,” alisema Rais Kenyatta.

 

Viongozi hao wawili walijadiliana juhudi za kimataifa za kukabiliana na ugaidi, mabadiliko ya hali ya hewa pamoja na biashara na uwekezaji miongoni mwa maswala mengine muhimu baina ya mataifa haya mawili.

 

Kiongozi huyo wa taifa alisema kuwa Kenya imepiga hatua kubwa katika kudhibiti na kukabiliana na mabadiliko ya hali ya anga huku akiikaribisha Marekani katika makubaliano ya Paris.

 

Mkutano huo wa White House ulikuwa kilele cha ziara rasmi iliyofana ya Rais  Kenyatta nchini marekani ambapo pia aliongoza mkutano wake wa kwanza wa baraza la usalama la umoja wa mataifa katika makao makuu ya umoja wa mataifa jijini New York.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad