Rais Ramaphosa Aruhusu Jeshi Kusimamia Uchaguzi Afrika Kusini





Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa ameruhusu kupelekwa kwa wanajeshi 10,000 kusimamia uchaguzi wa wiki ijayo wa serikali za mitaa, bunge limetangaza Jumatano.

Jeshi litasaidia polisi kuhakikisha kunakuwa na amani na mazingira ya usalama katika uchaguzi wa Jumatatu ambao utachagua madiwani na mameya kwa mujibu wa taarifa ya bunge la taifa.

Hatua hiyo ya uchaguzi imetokana na ghasia na wizi uliofanyika mwezi Julai kutokana na kufungwa jela rais wa zamani wa taifa hilo Jacob Zuma. Ghasia hizo ambazo hazijawahi kushuhudiwa ziliwazidi polisi, na kusababisha wanajeshi 25,000 kupelekwa kwenda kuzituliza. Awamu ya kwanza ya kupelekwa kwa jeshi mitaani itaanza Jumamosi, na watakuwepo kwa kipindi cha siku tano.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad