Rais Samia Awazawadia Viwanja Wachezaji Twiga Stars




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan amewapa zawadi wachezaji wa Timu ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars kufuatia ushindi walioupata na kuwafanya kushinda Kombe la COSAFA kwa wanawake dhidi ya Malawi.

 

Rais Samia ametoa zawadi hiyo leo, Jumatano, Oktoba 27, 2021 kwenye hafla ya kukabidhiwa kombe hilo na vijana hao ambayo imefanyika Ikulu jijini Dar es salaam.

 

“Niseme watoto wangu wa Twiga Stars mmenifanya nitembee kifua mbele. Niwapongeze Twiga Stars kwa kutuletea fahari kwa mara nyingine, hakika nyinyi ni mashujaa na majina yenu yatakaa kwenye vitabu vya historia ya nchi hii kwenye michezo.

 

“Mwanangu Fatuma Issa umecheza vizuri sana kama mchezaji wa zamani wa AC Milan, Gennaro Gattuso, namna ambavyo ulikuwa unacheza nafasi yako ya kiungo mkabaji, nenda kaba Tanzania ipande juu, nilivyoambiwa wewe ni beki sikuamini.’

 

“Taifa Stars kuna kipindi huko nyuma walishinda nikaona viongozi wanapambana na wakurugenzi hadi wakapewa viwanja, leo na mimi nalipa, ninawapa viwanja wachezaji wa Twiga Stars huko Dodoma ambako na mimi mama yenu naishi. Najua wengi kati yenu hamtajenga huko Dodoma, kwanza nawaomba mpokee hivi viwanja, mbeleni huko tutajua nini cha kufanya.” ~Rais Samia Suluhu Hassan.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad