RAIS Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba kuthibiti urasimu wa kupata msamaha wa kodi kwa vifaa na bidhaa zitakazoagizwa kutoka nje ya nchi katika miradi inayotekeleza chini ya mpango wa fedha zilizotolewa na Shirika la Fedha Duniani (IMF) kwa Tanzania. Anaripoti Mwandishi wetu (endelea)
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 10 Oktoba, 2021 jijini Dodoma wakati akizindua kampeni ya maendeleo kwa ustawi na mapambano ya UVIKO -19 ambao umetokana na mkopo nafuu wa Sh trilioni 1.3 uliotolewa na Shirika hilo la IMF.
“Nakuagiza kusimamia suala hili, kuwa mwepesi kutoa misamaha ya kodi kwa yale yatakayoagiza kuja kutumika kwenye miradi hii,” alisema.
Pia amemuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali na Mkaguzi wa ndani wa hesabu za serikali kufuatilia kwa karibu matumizi ya fedha hizo ili kuhakikisha zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa na thamani halisi yaani ‘value for money’