RAIS Samia Suluhu Hassan amemteua Jaji Mustapha Siyani kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Eliezer Felishi aliyeteuliwa kuwa Mwanasheria Mkuu.
Kabla ya uteuzi huo, Jaji Siyani alikuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Dodoma, taarifa iliyotolewa Oktoba 8, 2021 na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais (Ikulu), Jaffar Haniu imesema uteuzi huo umeanza Oktoba 7, 2021.
Jaji Siyani ndiye aliyekuwa akisimamia kesi ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe na wenzake watatu wanaokabiliwa na mashtaka sita yakiwemo ya kula njama na kufadhili fedha kwa ajili ya vitendo vya kigaidi.