STAA wa Manchester United na timu ya taifa ya England , Marcus Rashford ametunukiwa udaktari wa heshima na Chuo Kikuu cha Manchester kutokana na harakati zake zinazopinga ubaguzi, umasikini na njaa kwa watoto.
Rashford ameelezea jinsi anavyopambana kwa kushirikiana na Serikali ya Uingereza kuhakikisha wanawapatia chakula watoto wenye mazingira magumu.
“Mamilioni ya familia hapa Uingereza yalipoteza mwelekeo wa maisha na upatikanaji wa chakula, juhudi zimeonekana leo watato masikini wakisogea kwenda hatua nyingine, kwa sababu hiyo leo ni siku ya furaha kwangu,” amesema Rashford.
Awali Rashford alipaswa kutunukiwa cheo hicho mwezi Julai mwaka jana, ila kutokana na tatizo la virusi vya corona, hafla hiyo ilisitishwa.
Rashford 23, ameweka rekodi ya kuwa kijana mwenye umri mdogo kutunukiwa udaktari hivi karibuni alizungumza na Rais wa zamani wa Marekani Barack Obama.