Rubani Aliyepotea na Ndege, DC Mtatiro Afunguka





NDEGE ya Shirika la Uhifadhi Pams Foundation Aina ya Bathawk 5HWXO iliyokuwa ikisaidia kutafuta Faru Weusi katika Pori la Akiba la Selous Wilayani Tunduru Mkoani Ruvuma imepotea kwa siku 11 ikiwa na Rubani wake Bw. Samweli Gibuyi.

 

Tunaendelea kumtafuta rubani mtanzania Bw. Samweli Balina Gibuyi pamoja na ndege ndogo aina ya “BatHawk” yenye namba za usajili 5H-WXO inayomilikiwa na Shirika lisilo la Kiserikali (NGO) la Uhifadhi lijulikanalo kwa jina la “Protected Areas Management Solution Foundation maarufu kwa jina la “PAMS Foundation”.

 

Rubani Samweli Balina Gibuyi aliruka hapa TUNDURU na ndege hiyo siku ya Jumatatu tarehe 18/10/2021 majira ya saa tisa na dakika tisa (03:09pm) alasiri kuelekea Pori la Akiba Selous – Kanda ya Kingupira.

 

Ndege hiyo iliombwa na Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania – TAWA kupitia Shirika la Uhifadhi la Frankfurt Zoological Society (FZS) ili kusaidia katika zoezi linaloendelea la utafutaji wa Faru Weusi katika Pori
la Akiba Selous.

 

Rubani Samweli alitarajia kutua Kingupira saa 11.30 jioni siku hiyo hiyo lakini hakutua na tulianza juhudi za kumtafuta kwa kutumia ndege 5, helikopta 1 ya polisi na vikosi vya ardhini na vya mamlaka ya anga. Hadi leo (jana) Ijumaa 29 Oktoba 2021 hatujampata rubani Samwel wala ndege aliyokuwa akiiendesha.

 

Tunaendelea kuwaomba watanzania wote watakaokuwa na taarifa zozote zinazoweza kutusaidia tukampata rubani na ndege hii, watoe taarifa kwenye mamlaka za karibu na maeneo walipo. Tunaendelea kumwombea “SAM” apatikane akiwa salama.

 

Julius S. Mtatiro,
Mkuu wa Wilaya ya Tunduru,
Ruvuma.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad