Huduma za mitandao ya kijamii ya Facebook, WhatsApp na Instagram zimerejea baada ya kutopatikana kwa saa nane.
Kupitia taarifa ya Facebook imeeleza kuwa sababu ya kutoweka kwa mitandao hiyo ni mifumo kutofanya kazi.
Huduma zote tatu zinamilikiwa na Facebook na hazikuweza kupatikana kwenye wavuti au kwenye programu za simu za mkononi.
Taarifa zinaeleza kuwa kukatika kwa huduma hizo ni hitilafu kubwa zaidi kuwahi kutokea.
Katika taarifa hiyo iliyotumwa usiku wa kuamkia leo Jumanne Oktoba 5,2021 imesema mabadiliko mabaya ya usanifu yaliathiri zana na mifumo ya ndani ya kampuni hiyo.
Facebook ilituma ujumbe wa kuomba radhi kwa walioathirika kutokana na kutokupatikana kwa huduma zake za mitandao ya kijamii.