Sabaya afikishwa mahakamani tena kesi ya uhujumu uchumi





Aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha kuendelea kusikiliza ushahidi katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili na wenzake sita.
Sabaya na wenzake wamefikishwa mahakamani hapo saa 3:14 asubuhi leo Jumatano Oktoba 27, 2021 wakiwa katika ulinzi mkali.

Kesi ya Sabaya inasikilizwa na Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Patricia Kisinda na jamhuri inawakilishwa na mawakili wa Serikali waandamizi Felix Kwetukia, Ofmed Mtenga na Wakili wa Serikali, Neema Mbwana.

Kesi hiyo iliahirishwa Oktoba 22 baada ya shahidi wa Jamhuri kudai kusumbuliwa na tumbo.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 27,2021 watuhumiwa wengine ni Enock Mnkeni, Watson Mwahomange, John Aweyo, Sylvester Nyegu, Jackson Macha na Nathan Msuya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad