Sabaya Akutwa na Hatia “Sio Mimi, Nilitumwa, Nataka Kufunga Ndoa”





Ulinzi ukiwa umeimarishwa nje na ndani ya mahakama.

Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Arusha, Odira Amworo amesema hakuna shaka washitakiwa watatu walifika dukani kwa Mohamed Saad siku ya tukio.

 

Pia, amesema amethibitisha mshitakiwa wa kwanza Lengai Ole Sabaya na mshitakiwa wa pili Sylivester Nyegu walikuwa wanafahamiana.

 

Hakimu Omworo amesema hayo leo Ijumaa Oktoba 15, 2021 wakati akiendelea kuchambua hoja wakati akisima hukumu ya Sabaya na washitakiwa wenzake watatu.

 

Akiendelea kuchambua hukumu hiyo, Hakimu Omworo amesema kuwa imethibitika mshitakiwa wa kwanza alikuwa na bastola ndani na nje kulikuwa na watu wawili wenye silaha hivyo, hakuna shaka duka la shahidi wa kwanza lilivamiwa na watu wenye silaha na lilikuwa chini ya watu wenye silaha.

 

Hata hivyo, amesema hakuna silaha iliyotumika katika tukio hilo, hivyo hakuna shambulizi la kutumia silaha.

 

Aidha, Hakimu amesema kati ya mashahidi 11 waliotoa ushahidi wao dhidi ya Sabaya, ni mashaidi wawili tu ndio ambao ushahidi wao haukuwa na mashiko. 

 

Sabaya amekutwa na hatia, Hakimu anawapa nafasi watuhumiwa wajitetee ili Wapungiziwe adhabu…. Sabaya anaiomba mahakama imuonee huruma kwani sio yeye bali alikuwa anatekeleza maagizo ya Mamlaka yake ya Uteuzi, na ana mchumba walikuwa wafunge ndoa na mahari ameshalipa

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad