NASREDDINE Nabi, Kocha mkuu wa Yanga amesema kuwa mshambuliaji wake Fiston Mayele anahitaji muda kidogo ili aweze kuwa kwenye ubora ambao wengi wanahitaji kuona akiwa nao uwanjani.
Mayele anakumbukwa kwa kuwatungua watani zao wa jadi Simba kwenye mchezo wa ngao ya jamii na aliweka wazi kuwa anahitaji tuzo ya mfungaji bora kwenye ligi mpaka sasa akiwa amecheza mechi mbili na hajafunga.
Akizungumza na Championi Jumamosi Nabi, alisema kuwa hana tatizo na uwezo wa Mayele Pamoja na washmbuliaji wengine waliopo Yanga ni suala la muda tu.
“ikiwa utazungumzia kuhusu washambuliaji nitakuambia kwamba kuna makosa ambayo yanafanyika hasa katika kumalizia nafasi ambazo zinatengenezwa lakini haina maana kwamba hakuna ubora kwao.
Ukimtazama Mayele ni moja ya wachezaji ambao wanapenda kufunga hivyo anahitaji muda sawa ilivyo kwa wengine kama Makambo hawa wote wanahitaji muda ili waweze kuwa imara kwani maandalizi ya mwanzo hayakuwa mazuri kwetu.
Mechi ijayo kwa Yanga ni dhidi ya Kmc abayo inatarajiwa kuchezwa uwanja wa Majimaji Songea Oktoba 19.
STORI: LUNYAMADIZO MLYUKA