Sierra Leone imefuta rasmi adhabu ya kifo, baada ya Rais Julius Maada Bio kusaini muswada wa sheria mpya unaokataza adhabu ya kifo uliopitishwa na Bunge mwezi Julai.
"Kama taifa, leo tume tumeondoa hofu ya ukatili wa muda mrefu," alinukuliwa rais na shirika la AFP akizungumzia hatua hiyo.
"Leo tumethibitisha imani yetu kuhusu utakatifu wa maisha."
Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu lilisema kwamba mwaka jana kulikuwa na hukumu 39 za vifo.
Lakini hakuna mtu aliyenyongwa nchini Sierra Leone tangu mwaka 1998.
Adhabu ya kifo mara kadhaa zilibadilishwa, lakini mpaka kufikia mwishoni mwa mwaka jana, watu 94 walikuwa wanasubiri kunyongwa, Shirika la Amnesty lilisema.
Kwa mujibu wa gazeti la New York Times Sierra Leone inakuwa nchi ya 23 barani Afrika kuondoa adhabu ya kifo.