Simba Inapaswa Iombe Radhi Kwa Kauli za Mwijaku Leo Kuleta Mambo ya Ovyo na Faragha Kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari


Kwa miezi kadhaa sasa Simba ilishajijengea taswira yake baada ya kuondoka kwa Haji Manara aliyekuwa Msemaji lakini pia Muhamasishaji wa klabu hiyo.

Ilikuwa ni Simba yenye ukimya, inayosifiwa kwa uongozi bora na inayozidi kufanya vizuri, kilichokuwa kinasubiriwa ni kutangazwa kwa Msemaji na katika kipindi hicho ukitaka taarifa zake unapata kwenye akaunti zake za midandao ya kijamii mambo yanakwenda, na mashabiki walishazoea hali hiyo.

Lakini leo baada ya kuwatambulisha Wahamasishaji ghafla taswira imeyumba na kuvurugika kabisa, mmoja wa wahamasishaji 'Mwijaku' amekuja na kauli zisizo na weledi wala maadili, akitumia Mkutano wa Simba anakwambia Simba isiposhinda anavua nguo na kutembea uchi.

Kwa siku ya kwanza tu muhasishaji anaongelea mambo nyeti, ndoa ya mtu mwingine, anakwambia kama ndoa imemshinda atawezaje kuongoza timu. (akimlenga Manara).


Maneno hayo yamewakera mashabiki wa Simba lakini pia mashabiki wa soka kwa ujumla, na zaidi waandishi wa habari.

Unajua shida ni nini?, ni hivi maana yake ni kwamba kauli ya huyo muhamasishaji ndiyo kauli ya klabu, kwa kuwa ameyaongea kwenye mkutano wa klabu, hichi kitendo kimeshusha hadhi ya klabu.

Press ni kitu kikubwa sana, mambo yanayoongeleka hapo maana yake mlishayapanga kabla, pale mnakuja kuwasilisha tu.

HABARI KAMA HIZI DOWNLOAD APP YA UDAKU SPECIAL KWA KUBONYEZA > HAPA

Imekuwaje tena Simba inafanya mambo ya aibu kama haya, wakati ndiyo taswira ya soka la Tanzania kwa sasa?

Ushauri wangu ni, Kama Simba inamuhitaji muhamasishaji wake basi wamfundishe weledi alafu waombe radhi kwa kauli hizo.

@lemutuz_tv

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad